Kwa mujibu wa kifungu Na. 19 (2) (b) cha Sheria Na. 414, kutakuwa na Mkutano wa Taftishi siku ya Ijumaa, tarehe 16 Agosti 2019 katika Ukumbi wa New Faraja Villa uliopo Namtumbo Mjini kuanzia saa 4:00 asubuhi. Lengo la mkutano huo ni kupata maoni ya wadau ikiwa ni pamoja na Baraza la Ushauri la Serikali, Baraza la Ushauri la watumia huduma zinazodhibitiwa na EWURA, wateja wa Mamlaka ya Maji Namtumbo, na wananchi wote kwa ujumla kuhusu uhalali wa hoja za bei zinazopendekezwa. Soma Zaidi:-
Mwito wa Maoni ya Wadau-Namtumbo WSSA
A Call For Stakeholdres’ Views-Namtumbo WSSA
Views: 1344
Poleni na majukumu mimi fundi umeme daraja 1 ni hatua zipi nifate kupata leseni ya kazi?
Bwana Matonya, leseni inapatikana katika mfumo wa maombi ya leseni uitwao LOIS. Bofya kiunganishi Online Services kisha bofya LOIS kujisajili.
Hakikisha una nakala ya vyeti vyako zilizothibitishwa, picha ya pasipoti yenye kivuli cha bluu na wasifu wako (CV). Vyote hivi viwe katika nakala laini ili uweze kuvitumia unapofanya maombi mtandaoni.
Kwa maelezo zaidi piga 0800110030.
Karibu