Kwa mujibu wa kifungu Na. 19 (2) (b) cha Sheria Na. 414, EWURA inakaribisha maoni ya wadau wote kuhusu maombi ya Mamlaka ya Maji Tabora ya kurekebisha bei za maji kwa mwaka 2019/20-2022/23.
Wadau wanaopenda kutoa maoni wawasilishe maoni yao kwa njia ya barua pepe kwa anuani ya info@ewura.go.tz wakati wowote tangu tarehe ya tangazo hili.
Maoni kwa njia ya ujumbe wa maandishi au sauti kupitia mtandao wa WhatsApp, ujumbe wa simu ya mkononi au masanduku ya maoni yatapokelewa kuanzia tarehe 14 Aprili 2020.
Masanduku ya maoni yatawekwa katika ofisi za Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Tabora na Manispaa ya Tabora. Mwisho wa kuwasilisha maoni utakuwa tarehe 27 Aprili 2020.
Soma Zaidi:-
Mwito wa Maoni ya Wadau – Tabora WSSA
A Call for STAtakeholders’ Views – Tabora WSSA
Hits: 337