Kwa mujibu wa kifungu Na. 19 (2) (b) cha Sheria Na. 414, EWURA inakaribisha maoni ya wadau wote kuhusu maombi ya Mamlaka ya Maji Tabora. Wadau wanaopenda kutoa maoni wawasilishe maoni yao kwa njia ya barua pepe kwa anuani ya info@ewura.go.tz wakati wowote tangu tarehe ya tangazo hili.
Maoni kwa njia ya ujumbe wa maandishi au sauti kupitia mtandao wa WhatsApp na ujumbe wa simu ya mkononi yatapokelewa kupitia namba +255767610599 kuanzia tarehe 16 Aprili 2020. Aidha, tarehe hiyohiyo, masanduku ya maoni yatawekwa katika ofisi za Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Nzega na Halmashauri ya Mji wa Nzega. Mwisho wa kuwasilisha maoni itakuwa tarehe 27 Aprili 2020.
Soma Zaidi:Mwito wa Maoni ya Wadau -Nzega WSSA
Hits: 1471
Hi there, just wanted to say, I enjoyed this poѕt. It was funny.
Keep on posting!