Kwa mujibu wa kifungu Na. 19 (2) (b) cha Sheria Na. 414, EWURA inakaribisha maoni ya wadau wote kuhusu maombi ya Mamlaka ya Maji Tabora. Wadau wanaopenda kutoa maoni wawasilishe maoni yao kwa njia ya barua pepe kwa anuani ya info@ewura.go.tz wakati wowote tangu tarehe ya Tangazo hili. Maoni kwa njia ya ujumbe wa maandishi au sauti kupitia mtandao wa WhatsApp, ujumbe wa simu ya mkononi yatapokelewa kupitia namba +255 753 035 876 na +255 767 201 354 kuanzia tarehe 16 Aprili 2020. Aidha, tarehe hiyohiyo, masanduku ya maoni yatawekwa katika ofisi za Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Igunga na Halmashauri ya Wilaya ya Igunga. Mwisho wa kuwasilisha maoni utakuwa tarehe 27 Aprili 2020.
Soma Zaidi: Mwito wa Maoni ya Wadau- Igunga WSSA
Views: 311
Nimetumia unit 6 kwa mwezi bill niliyotumiwa ni sh 9,611.10 na sidaiwi je hiyo kwa sababu gani?
Ndugu Kafefa,
Tunakushauri ufike ofisi za TANESCO ili wakupatie ufafanuzi kuhusu suala hilo.
Karibu