Mtu yeyote atayekiuka Agizo hili atakuwa ametenda kosa kwa mujibu wa kifungu cha 238 cha sheria ya Petroli, Sura ya 392, na akipatikana na hatia adhabu yake ni faini si chini ya shilingi milioni 100 au kifungo cha miaka si chini ya 10 au vyote.
Soma Zaidi:-
Hits: 390
Hellow napenda kufahamu kuhusu fomu ya N-100
Ndugu Ahmed,
Fomu N-100 ni fomu ambayo inatumiwa na watoa huduma mbalimbali wazawa wenye makampuni kujisajili kutoa huduma katika miradi ya mafuta na gesi nchini ili kuweza kuingizwa katika kanzidata inayojulikana kama LSSP Database. Kanzidata hii inafanywa kwa mujibu wa sheria ya Petroli ya mwaka 2015 kwa lengo la kuwezesha kampuni za watanzania kutoa huduma husika katika miradi hiyo.
Fomu inapatikana katika kiunganishi https://www.ewura.go.tz/local-content-lssp-database/
Karibu