TAARIFA KWA UMMA :Mwito wa Maoni ya Wadau kuhusu Maombi ya Marekebisho ya Bei za Maji kutoka Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Orkesumet

Kwa mujibu wa kifungu Na. 19 (2) (b) cha Sheria Na. 414, kutakuwa na Mkutano wa Taftishi siku ya Alhamisi, tarehe 16 Februari 2022, katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Simanjiro, Orkesumet Mjini kuanzia saa 4:00 asubuhi kwa ajili ya kupata maoni ya wadau ikiwa ni pamoja na Baraza la Ushauri la Serikali, Baraza la Ushauri la Watumia Huduma Zinazodhibitiwa na EWURA (EWURA CCC) na wananchi wote kwa ujumla, kuhusu uhalali wa bei zinazopendekezwa. Wadau wanaombwa kuwasilisha maoni ya maandishi kwa Mkurugenzi Mkuu wa EWURA kupitia anuani iliyotajwa hapo juu wakati wowote hadi tarehe 23 Februari 2023.

Soma Zaidi:-Mwito wa Maoni ya Wadau Kuhusu Marekebisho ya Bei za Maji za Orkesumet WSSA

 

Hits: 159

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *