Tangazo hili limetolewa kwa mujibu wa Kifungu cha 19(4) cha Sheria ya EWURA Sura ya 414, ili kukusanya maoni kutoka kwa wadai ikiwa ni pamoja na Baraza la Ushauri la Serikali (EWURA GCC), Baraza Ushauri la Watumiaji wa Huduma Zinazodhibitiwa na EWURA (EWURA CCC), Wateja wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Lindi na umma kwa ujumla kuhusu bei zinazopendekezwa. Kama sehemu ya taftishi, kutakuwa na mkutano wa kusikiliza maoni ya wadau utakaofanyika siku ya Alhamisi, tarehe 8 Juni 2023 katika Ukumbi wa Double M iliopo Lindi mjini kuanzia saa nne asubuhi.
Soma Zaidi:-Mwito wa Maoni ya Wadau -Lindi WSSA
Views: 162