Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), inatangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli hapa nchini. Bei hizi zitaanza kutumika kuanzia Jumatano, Tarehe 6 Aprili 2022
Soma Zaidi:-https://www.ewura.go.tz/fuel-prices/
Hits: 20108
Nasikitika hapa kondoa vituo vya mafuta karibu vyote vinauza bei mpya kuanzia jioni hii,binafsi nimenunua Kwa bei mpya kabla tarehe iliyopendekezwa ,wahusika fuatilieni hili.
Ndugu Oswald,
Asante kwa taarifa.
Masuala hayo hufuatiliwa na hatua stahiki huchukuliwa.
Utakapokutana na masuala ya aina hiyo, tunakushauri uwe unatutumia risiti kwa wakati huo huo.
Karibu
Hata mimi nimeuziwa diesel kwa bei mpya maeneo korogwe tanga tanzania bei ya leo liter moja tsh 3276 na vijana wamenitumia ricti
Nasikitika hapa kondoa vituo vya mafuta karibu vyote vinauza bei mpya kuanzia jioni hii,binafsi nimenunua Kwa bei mpya kabla tarehe iliyopendekezwa ,wahusika fuatilieni hili.na risiti ninayo ambayo imebadilishwa mpaka saa inasoma saa 23:49:27 badala ya saa 19:46 niliponunua
Mliangalie vyema suala hili kwani limekuwa gumu sana kwa wengi
Nauliza waga mnatumia tasimin gani kupandisha mruta mbona kwenye NAURI mpo kmy sana
Jaman Tanzania ifanye uchunguzi wa kipato Cha raia wake maana mnapo pandisha Bei tunaumia sisi watu wa chini matajiri haliwafiki Hilo nasema hivi maana yanapopanda mafuta kila kitu kinapanda mtatuua kwa pressure
Nauliza waga mnatumia tasimin gani kupandisha mafumbona kwenye NAURI mpo kmy sana
Serikali inatakiwa ituangalie jamani hii kupanda kwamafuta imesha kua dili kwawengine
Jamani kwani iwe hivyo
Poleni sana EWURA kwa kazi ngumu na yenye maslahi mapana kwa Taifa.Hata hivyo ningependa kujua,ni kampuni gani inayoagiza mafuta kwa sasa.Kama sio TPDC kwa nini sio TPDC.Na je hatuoni kwamba kama TPDC ingeagiza mafuta yangekuwa rahisi zaidi,na wananchi wangepata mafuta na hata bidhaa kwa bei nafuu zaidi kuliko ilivyo sasa?
Ndugu Thomas,
Tafadhali rejea taarifa iliyotolewa na Waziri wa Nishati Bungeni, ambayo ina ufafanuzi wa suala uliloiliza.
Bofya kiunganishi hiki kusoma taarifa hiyo
Karibu.