MWITO WA MAONI: Maombi ya Marekebisho ya Bei ya Maji kutoka Majisafi na Usafi wa Mazingira Songea kwa Mwaka 2021/22 – 2023/24

TAARIFA inatolewa kwa umma kwamba, EWURA inawaalika wadau wote  na wananchi kwa ujumla katika  mkutano wa kusikiliza maoni ya wadau  siku ya Jumatatu, tarehe 22 Agosti 2022 katika Ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea kuanzia saa nne asubuhi kuhusu maombi ya marekebisho ya bei ya za maji kutoka Songea WSSA.

Maoni yanaweza kuwasilishwa kwa maandishi kwa Mkurugenzi Mkuu wa EWURA wakati wowote hadi tarehe 19 Agosti 2022 au Ofisi za EWURA Kanda ya Nyanda za Juu Kusini zilizopo  Mbeya Mjini au kwenye Ofisi za Mamlaka ya Maji Songea.

Soama Zaidi:-Marekebisho ya Bei -Songea WSSA

Visits: 516

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *