Taarifa hii inatolwa kwa mujibu wa Kifungu cha 19(4) cha Sheria ya EWURA Sura ya 414, kinachoitaka EWURA kutoa tangazo la taftishi ili kukusanya maoni kutoka kwa wadai ikiwa ni pamoja na Baraza la Ushauri la Serikali (EWURA GCC), Baraza Ushauri la Watumiaji wa Huduma Zinazodhibitiwa na EWURA (EWURA CCC), Wateja wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mbeya na Umma kwa ujumla kuhusu bei zinazopendekezwa. Kama sehemu ya taftishi, kutakuwa na mkutano wa kusikiliza maoni ya wadau utakaofanyika siku ya Alhamisi, tarehe 17 Novemba 2022 katika Ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya kuanzia saa nne asubuhi.
Soma Zaidi:-Mwito wa Maoni bei za Maji Mbeya WSSA
Views: 200